Cart

No products in the cart.

Shop

Makosa ya Kawaida katika Kiswahili
Makosa ya Kawaida katika Kiswahili
Sale

Makosa ya Kawaida katika Kiswahili

Makosa ya Kawaida katika Kiswahili ni mkusanyiko wa takribani maneno 2000 yanayotumiwa visivyo. Mapungufu hutokea kwa kutojua, kusahau na mazoea. Ukoseaji katika kuandika au kupiga chapa husababisha mategu. Kasoro hizo hukanganya maana ya maneno, sentensi au aya. Kimsingi, makosa huzuia uelewaji wa Kiswahili ongezi na andishi. Taksiri hizo hulemaza na kuchafua lugha sanifu. Madhumuni ya kitabu hiki ni kusahihisha aina za makosa ili kizazi cha elimu kisiyatumie kwa namna ghalati.
Original price was: KSh450.00.Current price is: KSh400.00.
Mizani
Mizani
Sale

Mizani

Mizani ni tamthilia kuhusu Mkwasi, mkewe Raufu pamoja na wanao (Nuru na Nuri). Wahusika hawa wanatofautishwa na imani zao. Mikondofikira na matamanio ya wahusika wakuu yanakinzana kama usiku na mchana. Mahusiano yao ya kijamii yanayumbishwa na utofauti wa imani na tamaduni. Mkwasi ni mganga na mtamaduni mkubwa aliyejizika katika mila na itikadi.
Original price was: KSh700.00.Current price is: KSh550.00.
My Mothers Tears
My Mothers Tears
Sale

My Mothers Tears

In "My Mother's Tears" the author embarks on a poignant journey through a decade of hardship and resilience. After leaving school, he confronts numerous challenges that shape his understanding of struggle and triumph. Through heartfelt narratives, the author shares his own trials and those of others, particularly his mother, whose unwavering strength inspires hope within their family and community. This collection of nonfiction explores the complexities of human emotion, focusing on themes of perseverance, love, and the indomitable spirit of those facing adversity.
Original price was: KSh480.00.Current price is: KSh450.00.
Samahani Na Hadithi Nyengine
Samahani Na Hadithi Nyengine
Sale

Samahani Na Hadithi Nyengine

Samahani na hadithi nyingine ni mkusanyiko wa hadithi zinazoangazia masuala mbalimbali katika jamii yetu. Waandishi wameonyesha upeo wa ubunifu kwa hadithi sisimuzi zilizoshiba mafunzo na maarifa. Matarajio yao ni kuwa wanafunzi wa sekondari na vyuoni watafaidi pakubwa.Sussy Nandama Sumbi, Timothy Omusikoyo Sumba na Kikechi Kombo ni weledi katika uhariri, uandishi na ufundishaji wa fasihi shuleni na vyuoni.
Original price was: KSh600.00.Current price is: KSh550.00.
Uhai Mwengine
Uhai Mwengine
Sale

Uhai Mwengine

"Mkosaji ni yeye mwenyewe! Anacho kisasi dhidi ya nafsi yake mwenyewe. Nafsi iliyomshinda kuidhibiti, ikamuangamiza .Hayo ndiyo machweo ya adhuhuri yaliyomchwea Mwanahalima na kuikatiza siku yake. Je, mwanaadamu anaweza kufa, afufuke na aishi uhai mwingine? Je uhai huu mwingine ni kama wa awali? Jamii nayo inaweza kufa, ikafufuka na kuishi uhai mwingine? Soma riwaya ya Uhai Mwingine ili ikufumbulie mafumbo mengi yaliyofumbatwa kifasihi.
Original price was: KSh480.00.Current price is: KSh450.00.
Usawiri chanya wa Hadhi ya Mwanamke katika Methali za Igikuria
Usawiri chanya wa Hadhi ya Mwanamke katika Methali za Igikuria
Sale

Usawiri chanya wa Hadhi ya Mwanamke katika Methali za Igikuria

Usawiri chanya wa Mwanamke katika Methali za Igikuria ni makala kwa ajili ya kumtukuza mwanamke katika jamii. Usawiri wa utukufu wa mwanamke katika methali za Igikuria umedadavuliwa huku mifano mwafaka ikitolewa. Kimsingi, mwanamke amemegewa nafasi yake katika ulimwengu wa sasa. Mwanamke anachangia pakubwa katika malezi na maendeleo ya jamii.
Original price was: KSh550.00.Current price is: KSh500.00.
Zambarau
Zambarau
SaleHot

Zambarau

Mheshimiwa Mwenyekiti anatawala wakazi wa Mibuyuni kwa udhalimu: Wananchi wanafanya maandamano ili kup-inga dhuluma zinazowafika ingawa wananyamazishwa na vyombo vya dola. Zema, mwanafunzi wa uanahabari anatumia vyombo kadha wa kadha kutetea haki za wanyonge ambao hawana sauti. . Matimaye, haki inashinda dhuluma wakati kiongozi mbaya (mheshimiwa Mwenyekiti) anabanduliwa madara-kani. Matarajio ya mwandishi ni kuwa wanafunzi wa sekondari watafaidi pakubwa. Tamthilia hii inazingatia matakwa ya mtalaa wa umilisi. Mwandishi wa tamthilia hii, Elishaphan Wachira (Jina Kubwa) ni ashiki wa Kiswahili ambaye ameandika tanzu mbalimbali za fasihi na lugha. Amesomea taaluma ya ualimu katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. Bwana Wachira ni mwalimu wa Kiswahili katika Shule ya Upili ya Mwan-gaza, Murang'a.
Original price was: KSh550.00.Current price is: KSh500.00.