Author
Mstahifu Mabruki almaarufu Ustadh Maalim ni mwalimu, mkalimani, mtafsiri, mhakiki, mnukuzi, mshaurinasaha na mchangiaji wa vipindi vya Kiswahili redioni. Amefunza somo la Kiswahili kwa zaidi ya miongo miwili. Amefunza katika Shule ya Lucina, St. Emma Academy, Shule ya Upili ya Pala, St. Mary's School Nairobi, Elijen Teachers Training College na shule nyinginezo. Amechangia katika vipindi vya Radio Maisha, Radio Waumini, Radio Milele FM, Radio Jambo, KBC Radio Taifa na Radio Qwetu. Sasa hivi, yeye ni mkurugenzi na mwasisi katika Kituo cha Lugha cha Afro-Nairobi (Afro Languages Centre). Kituo hiki cha Afro Languages Centre kinatoa huduma za tafsiri, ukalimani, ujanibishaji, unukuzi na mafunzo ya lugha ashirafu ya Kiswahili kwa wageni na wenyeji.
Mstahifu Mabruki
About Mstahifu Mabruki
Author Details
Books by Mstahifu Mabruki
1 published book