Mwenge wa Hadithi Fupi (Misingi na Nadharia)
by Fred C. N. W. Simiyu , Ernest Sangai Mohochi , Sanja Leo Leonard
Description
<span style="font-family:"Times New Roman",serif; mso-ansi-language:EN-GB">... Kuna idadi kubwa sana ya hadithi ambazo huachwa nje katika ufafanuzi kutokana na ufinye ambao nadharia ilivyo kijadi, imefanya zitupiliwe mbali na wahakiki, wasomi na wachapishaji (Carpenter na Neumeyer, 1974; Allen, 1981; Tindyebwa, 1988; Shaw 1983; De Grandsaigne, 1985 na Kibera, 1988). 
<span style="font-family:"Times New Roman",serif; mso-ansi-language:EN-GB">Hii ndio maana waandishi wa Mwenge wa Hadithi Fupi: Misingi na Nadharia wanabainisha uhusiano wa hadithi fupi na taaluma ya fasihi linganishi; pamoja na utokeaji wa hadithi fupi kama wasifu au otografia. Fauka ya hayo, Simiyu na wenzake wamepanua uwanda wa nadharia za ubunaji pamoja na za uhakiki wa fasihi. Maoni ni kwamba, watunzi huzingatia au huelekezwa na nadharia za utunzi, wakati mwingine bila kujua.
<span style="font-family:"Times New Roman",serif; mso-ansi-language:EN-GB"> Wahakiki nao hufanya kazi yao kwa kuongozwa na nadharia za uhakiki wa fasihi... Isitoshe, mawazo za waandishi kupitia wahakiki ndio huongoza maarifa ya kiusomi na ndiposa kuna maelezo kuhusu nadharia ambazo hazijatumika kwa mapana katika fasihi ya Kiswahili katika kitabu hiki. Nategetmea kitabu hiki kitatoa mwamko mpya wa kuwazia jinsi ambavyo utanzu huu umekukwa ukihakikiwa na hata kuwafaa waandishi hatimaye kubadilisha mitazamo na kunoa kalamu zao hata zaidi.<o:p></o:p>
<span style="font-family:"Times New Roman",serif; mso-ansi-language:EN-GB">Prof. R. M. Wafula, Chuo Kikuu cha Kenyatta, Juni 2026.<o:p></o:p>
<span style="font-family:"Times New Roman",serif; mso-ansi-language:EN-GB">Fred, C. N. W. Simiyu<span style="font-family:"Times New Roman",serif;mso-ansi-language:EN-GB"> ni msomi, mwalimu na mwandishi wa Fasihi, Tafsiri, Utamaduni na Lugha ya Kiswahili mwenye tajriba pana. Kufikia sasa, Simiyu ameandika hadhithi fupi tatu: Kisima chenye Hekima, Nizikeni Mtandaoni na Ulumbi wa Ipara. Kadhalika, amehariri diwani ya Kisima chenye Hekima na Hadithi Nyingine pamoja na Ulumbi wa Ipara na Hadithi Nyingine. 
<span style="font-family:"Times New Roman",serif;mso-ansi-language:EN-GB">Isitoshe, yeye ndiye Mhariri Mkuu wa TAALUMA, Jarida la CHAKITA. Aidha, Simiyu ndiye mwandishi wa Kitovu cha Fasihi Simulizi; Misingi ya Ukalimani na Tafsiri; Stadi za Mawasiliano na Mbinu za Kufundishia Kiswahili; Concise Trilingual English-Kiswahili-French Dictionary; Safina ya Utafiti wa Fasihi Simulizi; na Kiswahili na Uchumi wa Kidijitali. Kwa sasa, yeye ni Mwenyekiti wa CHAKITA na Mhadhiri Mwandamizi wa Taaluma za Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Kibabii, Bungoma - Kenya; na Mtafiti wa Lugha za Kiafrika katika the University of the Free State, South Africa.<o:p></o:p>
<span style="font-family:"Times New Roman",serif; mso-ansi-language:EN-GB">Ernest Sangai Mohochi<span style="font-family:"Times New Roman",serif;mso-ansi-language:EN-GB"> na Profesa wa Taaluma za Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Kibabii ambapo anahudumu pia kama Mkurugenzi wa Kituo cha Taaluma za Lugha na Utamaduni (KITALU). Mohochi amefundisha kozi mbalimbali za isimu na fasihi ya Kiswahili kwa zaidi ya miaka thelathini katika vyuo vikuu sita tofauti ndani na nje ya nchi ya Kenya. 
<span style="font-family:"Times New Roman",serif;mso-ansi-language:EN-GB">Miongoni mwa kozi alizozifundisha ni kozi ya Hadithi Fupi ya Kiswahili. Katika upande wa fasihi, Mohochi amebobea zaidi katika utanzu wa hadithi fupi. Sangai amechapisha hadithi fupi nne kufikia sasa: Ufunguo, Nilimwamini Baba, Uchachu Huja Baadaye na Kadhia za Maandamana. Aidha, Mohochi ameandika makala nne kuhusu hadithi fupi katika majarida mbalimbali.<o:p></o:p>
<span style="font-family:"Times New Roman",serif; mso-ansi-language:EN-GB">Sanja Leo Leonard<span style="font-family: "Times New Roman",serif;mso-ansi-language:EN-GB"> ni mwandishi na mhariri tajika wa hadithi fupi. Ndiye mhariri wa diwani ya Mwavyaji wa Roho na Hadithi nyingine, Alionja Asali na Hadithi Nyingine na Kisima chenye Hekima na Hadithi Nyingine. Sanja ndiye mwandishi wa hadithi fupi tano: Mimba Ingali Mimba, Kasalia, Kwekwe la Utumwa, Ndoto ya Pacha na Pachika na Sumu ya Neno. Kwa sasa, Sanja ni Mhadhiri wa Fasihi na Lugha katika Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Nairobi.<o:p></o:p>
<span style="font-family:"Times New Roman",serif; mso-ansi-language:EN-GB">ISBN<span style="font-family:"Times New Roman",serif; mso-ansi-language:EN-GB">: 978-9966-59-028-2<o:p></o:p>
About the Authors
Meet the authors behind this title
Reviews on Mwenge wa Hadithi Fupi (Misingi na Nadharia)
Explore authentic reader thoughts and share your own perspective.
You May Also Like
More titles from our catalog