TUNU Publishers

TUNU

Publishers

Your Selected Books

Subtotal: KES 0.00
Home Authors Rajabu Ali Mattaza
Author

Rajabu Ali Mattaza

About Rajabu Ali Mattaza

Rajabu Ali Mattaza almaarufu Rajabu Pilau, alizaliwa Takaungu, Kilifi mwaka wa 1943. Alikulia Takaungu na kujifunza ushairi kutoka kwa washairi wa zama hizo. Baadaye, alihamia Mombasa alikofanya kazi ya udereva. Kazini, alikutana na masogora wa Mombasa ambao walisifika kwa utunzi wa mashairi huku akilumbana nao. Alishiriki katika malumbano na alipendwa na kuheshimiwa na washairi wa Mombasa. Vilevile, Mzee Rajabu Ali Mattaza ameshiriki katika mahojiano katika tafiti mbalimbali za ushairi wa Kiswahili. Aghalabu, yeye huwashauri walimu na wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini Kenya. Sifa za utunzi wake zimezagaa katika miji ya pwani ya Kenya hadi visiwa vya Pemba.

Author Details

Books by Rajabu Ali Mattaza

1 published book